Agano la Kale

Agano Jipya

Mathayo 5:37-48 Biblia Habari Njema (BHN)

37. Ukisema, ‘Ndiyo’, basi iwe ‘Ndiyo’; ukisema, ‘Siyo’, basi iwe kweli ‘Siyo’. Chochote kinachozidi hayo hutoka kwa yule Mwovu.

38. “Mmesikia kwamba ilisemwa: ‘Jicho kwa jicho, jino kwa jino.’

39. Lakini mimi nawaambieni, usimlipize kisasi mtu mbaya. Mtu akikupiga kofi shavu la kulia, mgeuzie pia la pili.

40. Mtu akikupeleka mahakamani kutaka kukuchukulia shati lako, mwache achukue pia koti lako.

41. Mtu akikulazimisha kubeba mzigo wake kilomita moja, ubebe kilomita mbili.

42. Akuombaye mpe, wala usimpe kisogo anayetaka kukukopa kitu.

43. “Mmesikia kwamba ilisemwa: ‘Mpende jirani yako, na kumchukia adui yako.’

44. Lakini mimi nawaambieni, wapendeni maadui zenu na kuwaombea wale wanaowadhulumu nyinyi,

45. ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaangazia jua lake watu wabaya na wema, na kuwanyeshea mvua watu wanyofu na waovu.

46. Je, mtapata tuzo gani kwa kuwapenda tu wale wanaowapenda nyinyi? Hakuna! Kwa maana, hata watozaushuru hufanya hivyo!

47. Kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mmefanya kitu kisicho cha kawaida? Hata watu wasiomjua Mungu nao hufanya vivyo hivyo.

48. Basi, muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Kusoma sura kamili Mathayo 5