Agano la Kale

Agano Jipya

Mathayo 3:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Siku zile Yohane Mbatizaji alitokea, akaanza kuhubiri katika jangwa la Yudea:

2. “Tubuni, maana ufalme wa mbinguni umekaribia.”

3. Huyu Yohane ndiye yule ambaye nabii Isaya alinena juu yake aliposema:“Sauti ya mtu anaita jangwani:‘Mtayarishieni Bwana njia yake,nyosheni barabara zake.’”

4. Yohane alivaa vazi lililoshonwa kwa manyoya ya ngamia, na ukanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.

5. Basi, watu kutoka Yerusalemu, kutoka pande zote za Yudea na sehemu zote za kandokando ya mto Yordani, walimwendea,

6. wakaziungama dhambi zao, naye akawabatiza katika mto Yordani.

7. Lakini alipowaona Mafarisayo wengi na Masadukayo wanamjia ili awabatize, aliwaambia, “Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewadokezea muikimbie ghadhabu inayokuja?

8. Onesheni kwa vitendo kwamba mmetubu.

Kusoma sura kamili Mathayo 3