Agano la Kale

Agano Jipya

Mathayo 26:9-18 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Marashi haya yangaliweza kuuzwa kwa bei kubwa, maskini wakapewa hizo fedha.”

10. Yesu alitambua mawazo yao, akawaambia, “Mbona mnamsumbua huyu mama? Yeye amenitendea jambo jema.

11. Maskini mnao daima pamoja nanyi, lakini mimi sitakuwapo pamoja nanyi daima.

12. Huyu mama amenimiminia marashi ili kunitayarisha kwa maziko.

13. Nawaambieni kweli, popote ulimwenguni ambapo hii Habari Njema itahubiriwa, kitendo hiki alichofanya mama huyu kitatajwa kwa kumkumbuka yeye.”

14. Kisha, Yuda Iskarioti, mmoja wa wale kumi na wawili, akaenda kwa makuhani wakuu,

15. akawaambia, “Mtanipa kitu gani kama nikimkabidhi Yesu kwenu?” Wakamhesabia vipande thelathini vya fedha;

16. na tangu wakati huo Yuda akawa anatafuta nafasi ya kumsaliti.

17. Siku ya kwanza kabla ya sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, wanafunzi walimwendea Yesu wakamwuliza, “Unataka tukuandalie wapi chakula cha Pasaka?”

18. Yeye akawajibu, “Nendeni mjini kwa mwanamume fulani, mkamwambie: ‘Mwalimu anasema, wakati wangu umefika; kwako nitakula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu.’”

Kusoma sura kamili Mathayo 26