Agano la Kale

Agano Jipya

Mathayo 26:72-75 Biblia Habari Njema (BHN)

72. Petro akakana tena kwa kiapo: “Simjui mtu huyo.”

73. Baadaye kidogo, watu waliokuwa pale wakamwendea Petro, wakamwambia, “Hakika, wewe pia ni mmoja wao, maana msemo wako unakutambulisha.”

74. Hapo Petro akaanza kujilaani na kuapa akisema, “Simjui mtu huyo!” Mara jogoo akawika.

75. Petro akakumbuka maneno aliyoambiwa na Yesu: “Kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.” Basi, akatoka nje, akalia sana.

Kusoma sura kamili Mathayo 26