Agano la Kale

Agano Jipya

Mathayo 26:4-14 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Wakashauriana jinsi ya kumtia Yesu nguvuni kwa hila wamuue.

5. Lakini wakaamua jambo hilo lisifanyike wakati wa sikukuu, kusije kukatokea ghasia kati ya watu.

6. Yesu alipokuwa Bethania, nyumbani kwa Simoni, aitwaye Mkoma,

7. mama mmoja aliyekuwa na chupa ya alabasta yenye marashi ya thamani kubwa, alimjia pale mezani alipokuwa amekaa kula chakula, akammiminia hayo marashi kichwani.

8. Wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, “Ya nini hasara hii?

9. Marashi haya yangaliweza kuuzwa kwa bei kubwa, maskini wakapewa hizo fedha.”

10. Yesu alitambua mawazo yao, akawaambia, “Mbona mnamsumbua huyu mama? Yeye amenitendea jambo jema.

11. Maskini mnao daima pamoja nanyi, lakini mimi sitakuwapo pamoja nanyi daima.

12. Huyu mama amenimiminia marashi ili kunitayarisha kwa maziko.

13. Nawaambieni kweli, popote ulimwenguni ambapo hii Habari Njema itahubiriwa, kitendo hiki alichofanya mama huyu kitatajwa kwa kumkumbuka yeye.”

14. Kisha, Yuda Iskarioti, mmoja wa wale kumi na wawili, akaenda kwa makuhani wakuu,

Kusoma sura kamili Mathayo 26