Agano la Kale

Agano Jipya

Mathayo 24:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Yesu alitoka hekaluni, na alipokuwa akienda zake, wanafunzi wake walimwendea, wakamwonesha majengo ya hekalu.

2. Yesu akawaambia, “Sawa, mnaweza kuyatazama haya yote! Kweli nawaambieni, hakuna hata jiwe moja litakalosalia hapa juu ya lingine; kila kitu kitaharibiwa.”

3. Yesu alipokuwa ameketi juu ya mlima wa Mizeituni, wanafunzi walimwendea faraghani, wakamwuliza, “Tuambie mambo haya yatatukia lini? Ni ishara gani itakayoonesha kuja kwako na mwisho wa nyakati?”

4. Yesu akawajibu, “Jihadharini msije mkadanganywa na mtu.

5. Maana wengi watatokea wakisema kila mmoja kwamba yeye ndiye Kristo nao watawapotosha watu wengi.

6. Mtasikia juu ya vita na fununu za vita; lakini msifadhaike, maana hayo hayana budi kutokea, lakini mwisho wenyewe ungali bado.

7. Taifa moja litapigana na taifa lingine; ufalme mmoja utapigana na ufalme mwingine. Hapa na pale patakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi.

8. Yote hayo ni kama mwanzo wa maumivu ya kujifungua mtoto.

9. “Kisha watawatoeni ili mteswe na kuuawa. Mataifa yote yatawachukieni kwa sababu ya jina langu.

10. Tena, wengi wataiacha imani yao, watasalitiana na kuchukiana.

11. Watatokea manabii wengi wa uongo watakaowapotosha watu wengi.

12. Kwa sababu ya ongezeko la uhalifu, upendo wa watu wengi utafifia.

Kusoma sura kamili Mathayo 24