Agano la Kale

Agano Jipya

Mathayo 2:3-8 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, yeye pamoja na wakazi wote wa Yerusalemu.

4. Basi, akawaita pamoja makuhani wakuu wote na waalimu wa sheria, akawauliza, “Kristo atazaliwa wapi?”

5. Nao wakamjibu, “Mjini Bethlehemu, mkoani Yudea. Ndivyo nabii alivyoandika:

6. ‘Ee Bethlehemu nchini Yudea,wewe si mdogo kamwe kati ya miji maarufu ya Yudea;maana kwako atatokea kiongoziatakayewaongoza watu wangu, Israeli.’”

7. Hapo, Herode aliwaita faraghani hao wataalamu wa nyota, akawauliza wakati hasa ile nyota ilipowatokea.

8. Kisha akawatuma Bethlehemu akisema, “Nendeni mkachunguze kwa makini habari za mtoto huyo. Mkisha mpata nileteeni habari ili nami niende kumwabudu.”

Kusoma sura kamili Mathayo 2