Agano la Kale

Agano Jipya

Mathayo 17:2-8 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao, uso wake ukangaa kama jua na mavazi yake yakawa meupe kama mwanga.

3. Mose na Elia wakawatokea, wakawa wanazungumza naye.

4. Hapo Petro akamwambia Yesu, “Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa! Ukipenda nitajenga vibanda vitatu: Kimoja chako, kimoja cha Mose na kimoja cha Elia.”

5. Alipokuwa bado anasema hivyo, wingu jeupe likawafunika, na sauti ikasikika kutoka hilo wingu: “Huyu ni Mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye, msikilizeni.”

6. Wanafunzi waliposikia hivyo wakaanguka kifudifudi, wakaogopa sana.

7. Yesu akawaendea, akawagusa, akasema, “Simameni, msiogope!”

8. Walipoangalia juu hawakumwona mtu, ila Yesu peke yake.

Kusoma sura kamili Mathayo 17