Agano la Kale

Agano Jipya

Mathayo 14:24-36 Biblia Habari Njema (BHN)

24. na wakati huo ile mashua ilikwisha fika karibu katikati ya ziwa, lakini ilikumbwa na taabu kwa sababu upepo ulikuwa unaipinga.

25. Usiku, karibu na mapambazuko, Yesu aliwaendea wanafunzi akitembea juu ya maji.

26. Wanafunzi wake walipomwona akitembea juu ya maji waliogopa sana, wakasema, “Ni mzimu!” Wakapiga yowe kwa hofu.

27. Mara, Yesu akasema nao, “Tulieni, ni mimi. Msiogope!”

28. Petro akamwambia, “Bwana, ikiwa ni wewe kweli, amuru nitembee juu ya maji nije kwako.”

29. Yesu akasema, “Haya, njoo.” Basi, Petro akashuka kutoka ile mashua, akatembea juu ya maji, akamwendea Yesu.

30. Lakini alipouona ule upepo, aliogopa, akaanza kuzama; akalia kwa sauti, “Bwana, niokoe!”

31. Hapo, Yesu akaunyosha mkono wake, akamshika na kumwambia, “Ewe mwenye imani haba! Kwa nini uliona shaka?”

32. Kisha wakapanda mashuani, na upepo ukatulia.

33. Wote waliokuwa ndani ya mashua walimsujudia, wakasema, “Hakika wewe ni Mwana wa Mungu.”

34. Walivuka ziwa, wakafika nchi ya Genesareti.

35. Watu wa huko walipomtambua, wakaeneza habari pote katika sehemu hizo. Basi, wakamletea Yesu wagonjwa wote,

36. wakamwomba awaruhusu waguse tu pindo la vazi lake. Nao wote waliomgusa walipona.

Kusoma sura kamili Mathayo 14