Agano la Kale

Agano Jipya

Mathayo 12:14-26 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Basi, Mafarisayo wakatoka nje, wakashauriana jinsi watakavyomwangamiza Yesu.

15. Lakini Yesu alipojua jambo hilo, akatoka mahali pale. Watu wengi walimfuata, akawaponya wagonjwa wote,

16. akawaamuru wasiwaambie watu habari zake,

17. ili yale aliyosema Mungu kwa njia ya nabii Isaya yatimie:

18. “Tazama mtumishi wangu niliyemteua,mpendwa wangu anipendezaye moyoni.Nitaiweka roho yangu juu yake,naye atatangaza hukumu yangu kwa mataifa yote.

19. Hatakuwa na ubishi wala kupiga kelele,wala sauti yake haitasikika barabarani.

20. Mwanzi uliopondeka hatauvunja,wala utambi ufukao moshi hatauzima,mpaka atakapoifanya hukumu ya haki itawale.

21. Kwake yeye mataifa yatakuwa na matumaini.”

22. Hapo watu wakamletea Yesu mtu mmoja kipofu na ambaye alikuwa bubu kwa sababu alikuwa amepagawa na pepo. Yesu akamponya hata akaweza kusema na kuona.

23. Umati wote wa watu ulishangaa ukasema, “Je, huenda ikawa huyu ndiye Mwana wa Daudi?”

24. Lakini Mafarisayo waliposikia hayo, wakasema, “Mtu huyu anawafukuza pepo kwa uwezo wa Beelzebuli, mkuu wa pepo.”

25. Yesu, akiwa anayajua mawazo yao, akawaambia, “Ufalme wowote uliogawanyika makundimakundi yanayopingana, hauwezi kudumu, na mji wowote au jamaa yoyote iliyogawanyika makundimakundi yanayopingana, itaanguka.

26. Ikiwa Shetani anamfukuza Shetani, anajipinga mwenyewe. Basi, ufalme wake utasimamaje?

Kusoma sura kamili Mathayo 12