Agano la Kale

Agano Jipya

Matendo 7:45-57 Biblia Habari Njema (BHN)

45. Kisha babu zetu walilipokezana wao kwa wao mpaka wakati wa Yoshua, walipoinyakua ile nchi kutoka kwa mataifa ambayo Mungu aliyafukuza mbele yao. Hapo lilikaa mpaka nyakati za Daudi.

46. Daudi alipata upendeleo kwa Mungu, akamwomba Mungu ruhusa ya kumjengea makao yeye aliye Mungu wa Yakobo.

47. Lakini Solomoni ndiye aliyemjengea Mungu nyumba.

48. “Hata hivyo, Mungu Mkuu haishi katika nyumba zilizojengwa na binadamu; kama nabii asemavyo:

49. ‘Bwana asema:Mbingu ni kiti changu cha enzina dunia ni kiti changu cha kuwekea miguu.

50. Ni nyumba ya namna gani basi mnayoweza kunijengea,na ni mahali gani nitakapopumzika?Vitu hivi vyote ni mimi nimevifanya, au sivyo?’

51. “Enyi wakaidi wakuu! Mioyo na masikio yenu ni kama ya watu wa mataifa. Nyinyi ni kama babu zenu. Siku zote mnampinga Roho Mtakatifu.

52. Je, yuko nabii yeyote ambaye babu zenu hawakumtesa? Waliwaua hao Mungu aliowatuma watangaze kuja kwake yule Mwenye Haki. Na sasa, nyinyi mmemsaliti, mkamuua.

53. Nyinyi mliipokea ile sheria iliyoletwa kwenu na Malaika, lakini hamkuitii.”

54. Wale wazee wa Baraza waliposikia hayo, walighadhibika sana, wakamsagia meno kwa hasira.

55. Lakini Stefano akiwa amejawa na Roho Mtakatifu, akatazama juu mbinguni, akauona utukufu wa Mungu na Yesu amekaa upande wa kulia wa Mungu.

56. Akasema, “Tazameni! Ninaona mbingu zimefunuliwa na Mwana wa Mtu amesimama upande wa kulia wa Mungu.”

57. Hapo, watu wote katika kile kikao cha Baraza, wakapiga kelele na kuziba masikio yao kwa mikono yao. Kisha wakamrukia wote kwa pamoja,

Kusoma sura kamili Matendo 7