Agano la Kale

Agano Jipya

Matendo 7:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Basi, kuhani mkuu akamwuliza, “Je, mambo haya ni kweli?”

2. Naye Stefano akasema, “Ndugu zangu na akina baba, nisikilizeni! Mungu alimtokea babu yetu Abrahamu alipokuwa kule Mesopotamia kabla hajaenda kukaa kule Harani.

3. Mungu alimwambia: ‘Ondoka katika nchi yako; waache watu wa ukoo wako; nenda katika nchi nitakayokuonesha!’

4. Kwa hivyo, Abrahamu alihama nchi ya Kaldayo, akaenda kukaa Harani. Baada ya kifo cha baba yake, Mungu alimtoa tena Harani akaja kukaa katika nchi hii mnayokaa sasa.

Kusoma sura kamili Matendo 7