Agano la Kale

Agano Jipya

Matendo 16:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Paulo alifika Derbe na Lustra, ambako aliishi mfuasi mmoja aitwaye Timotheo. Mama yake ambaye pia alikuwa mfuasi, alikuwa Myahudi; lakini baba yake alikuwa Mgiriki.

2. Timotheo alikuwa na sifa kubwa kati ya wale ndugu wa Lustra na Ikonio.

3. Paulo alitaka Timotheo aandamane naye safarini, kwa hiyo alimtahiri. Alifanya hivyo kwa sababu Wayahudi wote walioishi sehemu hizo walijua kwamba baba yake Timotheo alikuwa Mgiriki.

Kusoma sura kamili Matendo 16