Agano la Kale

Agano Jipya

Matendo 12:21-25 Biblia Habari Njema (BHN)

21. Siku moja iliyochaguliwa, Herode akiwa amevaa mavazi rasmi na kuketi katika kiti cha kifalme, aliwahutubia watu.

22. Wale watu walimpigia kelele za shangwe wakisema, “Hii ni sauti ya mungu, si ya mtu.”

23. Papo hapo malaika wa Bwana akamwangusha Herode chini kwa sababu hakumpa Mungu hizo sifa. Akaliwa na wadudu, akafa.

24. Neno la Mungu likazidi kuenea na kukua.

25. Baada ya Barnaba na Saulo kutekeleza huduma yao, walitoka tena Yerusalemu, wakamchukua Yohane aitwaye pia Marko.

Kusoma sura kamili Matendo 12