1. Karibu wakati huohuo, mfalme Herode alianza kuwatesa baadhi ya Wakristo.
2. Alimuua kwa upanga Yakobo, ndugu yake Yohane.
3. Alipoona kuwa kitendo hicho kiliwapendeza Wayahudi, aliendelea, akamkamata Petro. (Hiyo ilifanyika wakati wa sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu).