Agano la Kale

Agano Jipya

Matendo 11:1-14 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mitume na ndugu kule Yudea walisikia kwamba watu wa mataifa mengine pia walikuwa wamelipokea neno la Mungu.

2. Basi, Petro aliporudi Yerusalemu, wale Wayahudi waumini waliopendelea watu wa mataifa mengine watahiriwe, walimlaumu wakisema:

3. “Wewe umekwenda kukaa na watu wasiotahiriwa na hata umekula pamoja nao!

4. Hapo Petro akawaeleza kinaganaga juu ya yale yaliyotendeka tangu mwanzo:

5. “Siku moja nikiwa nasali mjini Yopa, niliona maono; niliona kitu kama shuka kubwa ikishushwa chini kutoka mbinguni ikiwa imeshikwa pembe zake nne, ikawekwa kando yangu.

6. Nilichungulia ndani kwa makini nikaona wanyama wenye miguu minne, wanyama wa mwituni, wanyama watambaao na ndege wa angani.

7. Kisha nikasikia sauti ikiniambia: ‘Petro amka, chinja, ule.’

8. Lakini mimi nikasema: ‘La, Bwana; maana chochote kilicho najisi au kichafu hakijapata kamwe kuingia kinywani mwangu.’

9. Ile sauti ikasikika tena kutoka mbinguni: ‘Usiviite najisi vitu ambavyo Mungu amevitakasa.’

10. Jambo hilo lilifanyika mara tatu, na mwishowe vyote vilirudishwa juu mbinguni.

11. Ghafla, watu watatu waliokuwa wametumwa kwangu kutoka Kaisarea waliwasili kwenye nyumba nilimokuwa nakaa.

12. Roho aliniambia niende pamoja nao bila kusita. Hawa ndugu sita waliandamana nami pia kwenda Kaisarea na huko tuliingia nyumbani mwa Kornelio.

13. Yeye alitueleza jinsi alivyokuwa amemwona malaika amesimama nyumbani mwake na kumwambia: ‘Mtume mtu Yopa akamwite mtu mmoja aitwaye Simoni, kwa jina lingine Petro.

14. Yeye atakuambia maneno ambayo kwayo wewe na jamaa yako yote mtaokolewa.’

Kusoma sura kamili Matendo 11