Agano la Kale

Agano Jipya

Marko 6:39-55 Biblia Habari Njema (BHN)

39. Basi, Yesu akawaamuru wanafunzi wawaketishe watu wote makundimakundi penye nyasi.

40. Nao wakaketi makundimakundi ya watu 100 na ya watu hamsini.

41. Kisha Yesu akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akavibariki, akaimega mikate, akawapa wanafunzi wake wawagawie watu. Na wale samaki wawili pia akawagawia wote.

42. Watu wote wakala, wakashiba.

43. Wakaokota mabaki ya mikate na samaki pia, wakajaza vikapu kumi na viwili.

44. Nao waliokula hiyo mikate walikuwa wanaume 5,000.

45. Mara Yesu akawaamuru wanafunzi wake wapande mashua, wamtangulie kwenda Bethsaida, ngambo ya ziwa, wakati yeye anauaga umati wa watu.

46. Baada ya kuwaaga watu alikwenda mlimani kusali.

47. Ilipokuwa jioni, mashua ilikuwa katikati ya ziwa, naye alikuwa peke yake katika nchi kavu.

48. Basi, akawaona wanafunzi wake wakitaabika kwa kupiga makasia, maana upepo ulikuwa unawapinga. Karibu na mapambazuko, Yesu aliwaendea wanafunzi akitembea juu ya maji, akataka kuwapita.

49. Lakini walipomwona akitembea juu ya maji, walidhani ni mzimu, wakapiga yowe.

50. Maana wote walipomwona waliogopa sana. Mara Yesu akasema nao, “Tulieni, ni mimi. Msiogope!”

51. Kisha akapanda mashuani walimokuwa, na upepo ukatulia. Nao wakashangaa sana,

52. kwa sababu hawakuwa bado wameelewa maana ya ile mikate. Akili zao zilikuwa bado zimepumbazika.

53. Walivuka ziwa, wakafika nchi ya Genesareti, wakatia nanga.

54. Walipotoka mashuani watu walimtambua Yesu mara.

55. Basi, kwa haraka wakazunguka katika nchi ile yote, wakaanza kuwachukua wagonjwa wamelala juu ya mikeka yao, wakawapeleka kila mahali waliposikia Yesu yupo.

Kusoma sura kamili Marko 6