Agano la Kale

Agano Jipya

Marko 6:34-45 Biblia Habari Njema (BHN)

34. Aliposhuka pwani, Yesu aliona umati mkubwa wa watu, akawaonea huruma, kwa sababu walikuwa kama kondoo wasio na mchungaji. Akaanza kuwafundisha mambo mengi.

35. Saa za mchana zilikwisha pita. Basi, wanafunzi wakamwendea Yesu, wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na sasa kunakuchwa.

36. Afadhali uwaage watu waende mashambani na katika vijiji vya jirani, wanunue chakula.”

37. Lakini Yesu akawaambia, “Wapeni nyinyi chakula.” Nao wakamwuliza, “Je, twende kununua mikate kwa fedha dinari 200, na kuwapa chakula?”

38. Yesu akawauliza, “Mnayo mikate mingapi? Nendeni kutazama.” Walipokwisha tazama, wakamwambia, “Kuna mikate mitano na samaki wawili.”

39. Basi, Yesu akawaamuru wanafunzi wawaketishe watu wote makundimakundi penye nyasi.

40. Nao wakaketi makundimakundi ya watu 100 na ya watu hamsini.

41. Kisha Yesu akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akavibariki, akaimega mikate, akawapa wanafunzi wake wawagawie watu. Na wale samaki wawili pia akawagawia wote.

42. Watu wote wakala, wakashiba.

43. Wakaokota mabaki ya mikate na samaki pia, wakajaza vikapu kumi na viwili.

44. Nao waliokula hiyo mikate walikuwa wanaume 5,000.

45. Mara Yesu akawaamuru wanafunzi wake wapande mashua, wamtangulie kwenda Bethsaida, ngambo ya ziwa, wakati yeye anauaga umati wa watu.

Kusoma sura kamili Marko 6