Agano la Kale

Agano Jipya

Marko 5:9-17 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Basi, Yesu akamwuliza, “Jina lako nani?” Naye akajibu, “Jina langu ni ‘Jeshi,’ maana sisi tu wengi.”

10. Kisha akamsihi Yesu asiwafukuze hao pepo katika nchi ile.

11. Kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe malishoni kwenye mteremko wa mlima.

12. Basi, hao pepo wakamsihi, “Utupeleke kwa hao nguruwe, tuwaingie.”

13. Naye akawaruhusu. Basi, hao pepo wachafu wakatoka, wakawaingia wale nguruwe. Kundi lote la nguruwe wapatao 2,000 likaporomoka kwenye ule mteremko mkali mpaka ziwani, likatumbukia majini.

14. Wachungaji wa hao nguruwe walikimbia, wakatangaza jambo hilo mjini na mashambani. Watu wakafika kuona yaliyotukia.

15. Wakamwendea Yesu, wakamwona na mtu yuleyule aliyekuwa amepagawa na jeshi la pepo ameketi chini, amevaa nguo na ana akili yake sawa, wakaogopa.

16. Watu walioshuhudia tukio hilo wakawaeleza wengine mambo yaliyompata huyo mtu aliyekuwa amepagawa na pepo na juu ya wale nguruwe.

17. Basi, wakaanza kumwomba aondoke katika nchi yao.

Kusoma sura kamili Marko 5