Agano la Kale

Agano Jipya

Marko 4:1-14 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Yesu alianza kufundisha tena akiwa kando ya ziwa. Umati mkubwa wa watu ulimzunguka hata ikambidi aingie katika mashua na kuketi. Watu wote wakawa wamekaa katika nchi kavu, kando ya ziwa.

2. Aliwafundisha mambo mengi kwa mifano, na katika mafundisho yake aliwaambia,

3. “Sikilizeni! Mpanzi alikwenda kupanda mbegu.

4. Alipokuwa akipanda mbegu, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja wakazila.

5. Nyingine zilianguka penye mawe pasipokuwa na udongo mwingi, zikaota mara kwa kuwa udongo haukuwa na kina.

6. Jua lilipochomoza, zikateketea; na kwa kuwa mizizi yake haikuwa na nguvu, zikanyauka.

7. Nyingine zilianguka kwenye miti ya miiba, nayo ikakua na kuzisonga, nazo hazikuzaa nafaka.

8. Nyingine zilianguka katika udongo mzuri, zikamea, zikakua na kuzaa: Moja punje thelathini, moja sitini na nyingine mia.”

9. Kisha akawaambia, “Mwenye masikio na asikie!”

10. Yesu alipokuwa peke yake, baadhi ya wale waliomsikia walimwendea pamoja na wale kumi na wawili, wakamwuliza juu ya hiyo mifano.

11. Naye akawaambia, “Nyinyi mmejaliwa kujua siri ya ufalme wa Mungu, lakini wale walio nje wataambiwa kila kitu kwa mifano,

12. ili,‘Watazame kweli, lakini wasione.Wasikie kweli, lakini wasielewe.La sivyo, wangemgeukia Mungu,naye angewasamehe.’”

13. Basi, Yesu akawauliza, “Je, nyinyi hamwelewi mfano huu? Mtawezaje basi, kuelewa mfano wowote?

14. Mpanzi hupanda neno la Mungu.

Kusoma sura kamili Marko 4