Agano la Kale

Agano Jipya

Marko 14:56-64 Biblia Habari Njema (BHN)

56. Watu wengi walitoa ushahidi wa uongo juu ya Yesu, lakini ushahidi wao haukupatana.

57. Kisha wengine walisimama, wakatoa ushahidi wa uongo wakisema:

58. “Tulimsikia mtu huyu akisema, ‘Nitaliharibu hekalu hili lililojengwa kwa mikono, na kwa siku tatu nitajenga lingine lisilojengwa kwa mikono.’”

59. Lakini hata hivyo, ushahidi wao haukupatana.

60. Basi, kuhani mkuu akasimama katikati yao, akamwuliza Yesu, “Je, hujibu neno? Watu hawa wanashuhudia nini dhidi yako?”

61. Lakini yeye akakaa kimya; hakusema hata neno moja. Kuhani mkuu akamwuliza tena, “Je, wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu Mtukufu?”

62. Yesu akajibu, “Naam, mimi ndiye. Tena, mtamwona Mwana wa Mtu amekaa upande wa kulia wa yule Bwana Mwenye Nguvu, akija katika mawingu ya mbinguni.”

63. Hapo kuhani mkuu akararua joho lake, akasema, “Tuna haja gani tena ya mashahidi?

64. Mmesikia kufuru yake! Nyinyi mwaonaje?” Wote wakaamua kwamba anastahili kuuawa.

Kusoma sura kamili Marko 14