Agano la Kale

Agano Jipya

Marko 14:33-39 Biblia Habari Njema (BHN)

33. Kisha akawachukua Petro, Yakobo na Yohane; akaanza kufadhaika sana na kuhangaika.

34. Akawaambia, “Nina huzuni kubwa moyoni hata karibu kufa. Kaeni hapa na kukesha.”

35. Akaenda mbele kidogo, akajitupa chini kifudifudi, akasali kwamba, kama ingewezekana, asiipitie saa hiyo ya mateso.

36. Akasema, “Baba yangu, kwako mambo yote yanawezekana. Uniondolee kikombe hiki; lakini isiwe kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe.”

37. Kisha akarudi kwa wanafunzi wale watatu, akawakuta wamelala. Basi, akamwuliza Petro, “Simoni, je, umelala? Hukuweza kukesha hata saa moja?”

38. Kisha akawaambia, “Kesheni na kusali ili msije mkaingia katika majaribu. Roho inataka, lakini mwili ni dhaifu.”

39. Akaenda kusali tena akirudia maneno yaleyale.

Kusoma sura kamili Marko 14