Agano la Kale

Agano Jipya

Marko 10:6-11 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Lakini tangu kuumbwa ulimwengu, Mungu aliumba mwanamume na mwanamke.

7. Hivyo mwanamume atawaacha baba yake na mama yake, ataungana na mke wake,

8. nao wawili watakuwa mwili mmoja. Kwa hiyo, wao si wawili tena bali mwili mmoja.

9. Basi, alichounganisha Mungu, binadamu asitenganishe.”

10. Walipoingia tena ndani ya nyumba, wanafunzi wake walimwuliza juu ya jambo hilo.

11. Naye akawaambia, “Anayemwacha mkewe na kuoa mwingine, anazini dhidi ya mkewe.

Kusoma sura kamili Marko 10