Agano la Kale

Agano Jipya

Marko 10:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Yesu alitoka hapo akaenda mkoani Yudea, hata ngambo ya mto Yordani. Umati wa watu ukamwendea tena, naye akawafundisha tena kama ilivyokuwa desturi yake.

2. Basi, Mafarisayo wakamwendea, na kwa kumjaribu wakamwuliza, “Je, ni halali mume kumpa mkewe talaka?”

3. Yesu akawajibu, “Mose aliwapa maagizo gani?”

4. Nao wakasema, “Mose aliagiza mume kumpatia mkewe hati ya talaka na kumwacha.”

Kusoma sura kamili Marko 10