Agano la Kale

Agano Jipya

Luka 24:46-53 Biblia Habari Njema (BHN)

46. Akawaambia, “Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na siku ya tatu atafufuka kutoka kwa wafu,

47. na kwamba ni lazima, kwa jina lake, mataifa yote kuanzia Yerusalemu, yahubiriwe kwamba watu wanapaswa kutubu na kusamehewa dhambi.

48. Nyinyi ni mashahidi wa mambo hayo.

49. Nami mwenyewe nitawapelekeeni yule ambaye Baba aliahidi kumtuma, lakini ngojeni huku mjini mpaka mtakapopewa ile nguvu itokayo juu.”

50. Kisha akawaongoza nje ya mji hadi Bethania, akainua mikono yake juu, akawabariki.

51. Alipokuwa anawabariki, akawaacha; akachukuliwa mbinguni.

52. Wao wakamwabudu, kisha wakarudi Yerusalemu wakiwa na furaha kubwa:

53. Wakakaa muda wote hekaluni wakimsifu Mungu.

Kusoma sura kamili Luka 24