Agano la Kale

Agano Jipya

Luka 24:26-35 Biblia Habari Njema (BHN)

26. Je, haikumpasa Kristo kuteswa, na hivyo aingie katika utukufu wake?”

27. Akawafafanulia mambo yote yaliyomhusu yeye katika Maandiko Matakatifu kuanzia Mose hadi manabii wote.

28. Walipokikaribia kile kijiji walichokuwa wanakiendea, Yesu akafanya kana kwamba anaendelea na safari;

29. lakini wao wakamsihi wakisema, “Kaa pamoja nasi, maana kunakuchwa, na usiku unakaribia.” Basi, akaingia kijijini, akakaa pamoja nao.

30. Alipoketi kula chakula pamoja nao, akachukua mkate, akaubariki, akaumega, akawapa.

31. Mara macho yao yakafumbuliwa, wakamtambua; lakini yeye akatoweka kati yao.

32. Basi, wakaambiana, “Je, mioyo yetu haikuwa inawaka ndani yetu wakati alipokuwa anatufafanulia Maandiko Matakatifu kule njiani?”

33. Wakaondoka saa ileile, wakarudi Yerusalemu; wakawakuta wale mitume kumi na mmoja na wale wengine waliokuwa pamoja nao wamekusanyika

34. wakisema, “Hakika Bwana amefufuka, amemtokea Simoni.”

35. Basi, hao wafuasi wawili wakawajulisha yale yaliyowapata njiani, na jinsi walivyomtambua katika kumega mkate.

Kusoma sura kamili Luka 24