Agano la Kale

Agano Jipya

Luka 23:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kisha, wote kwa jumla, wakasimama, wakampeleka Yesu mbele ya Pilato.

2. Wakaanza kumshtaki wakisema: “Tulimkuta mtu huyu akiwapotosha watu wetu, akipinga kulipa kodi kwa Kaisari na kujiita ati yeye ni Kristo, Mfalme.”

3. Pilato akamwuliza Yesu, “Wewe ni Mfalme wa Wayahudi?” Yesu akamjibu, “Wewe umesema.”

4. Pilato akawaambia makuhani wakuu na umati wa watu, “Sioni kosa lolote katika mtu huyu.”

Kusoma sura kamili Luka 23