Agano la Kale

Agano Jipya

Luka 22:10-18 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Akawaambia, “Sikilizeni! Mtakapokuwa mnakwenda mjini, mtakutana na mwanamume anayebeba mtungi wa maji. Mfuateni mpaka ndani ya nyumba atakayoingia.

11. Mwambieni mwenye nyumba: ‘Mwalimu anakuuliza, kiko wapi kile chumba ambamo nitakula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu?’

12. Naye atawaonesheni chumba kikubwa ghorofani ambacho kimepambwa. Andalieni humo.”

13. Basi, wakaenda, wakakuta kila kitu sawa kama Yesu alivyokuwa amewaambia; wakaandaa karamu ya Pasaka.

14. Saa ilipotimia, Yesu akakaa kula chakula pamoja na mitume wake.

15. Akawaambia, “Nimetamani sana kula Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu.

16. Maana nawaambieni, sitaila tena hadi hapo itakapokamilika katika ufalme wa Mungu.”

17. Kisha akatwaa kikombe cha divai, akashukuru, akasema, “Pokeeni, mgawane.

18. Kwa maana nawaambieni, sitakunywa tena divai ya zabibu mpaka ufalme wa Mungu utakapokuja.”

Kusoma sura kamili Luka 22