Agano la Kale

Agano Jipya

Luka 22:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, iitwayo Pasaka, ilikuwa inakaribia.

2. Makuhani wakuu na waalimu wa sheria wakawa wanatafuta njia ya kumwua Yesu, lakini waliwaogopa watu.

3. Basi, Shetani akamwingia Yuda aitwaye Iskarioti, mmoja wa wale mitume kumi na wawili.

4. Yuda akaenda, akajadiliana na makuhani wakuu na walinzi wa hekalu kuhusu atakavyomsaliti Yesu kwao.

5. Nao wakafurahi na kupatana naye kumlipa fedha.

6. Yuda akakubali, na akawa anatafuta nafasi nzuri ya kumkabidhi kwao bila umati wa watu kujua.

7. Basi, siku ya mikate isiyotiwa chachu ikafika. Hiyo ndiyo siku ambayo mwanakondoo wa Pasaka huchinjwa.

8. Hivyo Yesu akawatuma Petro na Yohane, akawaambia, “Nendeni mkatuandalie karamu ili tupate kula Pasaka.”

Kusoma sura kamili Luka 22