Agano la Kale

Agano Jipya

Luka 2:5-11 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Alikwenda kuhesabiwa pamoja na mchumba wake Maria ambaye alikuwa mjamzito.

6. Walipokuwa huko, siku yake ya kujifungua ikawadia,

7. akajifungua mtoto wake wa kwanza wa kiume, akamvika nguo za kitoto, akamlaza horini kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.

8. Katika sehemu hizo, walikuwako wachungaji wakikesha usiku mbugani kulinda mifugo yao.

9. Malaika wa Bwana akawatokea ghafla, na utukufu wa Bwana ukawaangazia pande zote. Wakaogopa sana.

10. Malaika akawaambia, “Msiogope! Nimewaleteeni habari njema ya furaha kubwa itakayowapata watu wote.

11. Kwa maana, leo hii katika mji wa Daudi, amezaliwa Mwokozi kwa ajili yenu, ndiye Kristo Bwana.

Kusoma sura kamili Luka 2