Agano la Kale

Agano Jipya

Luka 19:32-45 Biblia Habari Njema (BHN)

32. Basi, wakaenda, wakakuta sawa kama alivyowaambia.

33. Walipokuwa wanamfungua yule mwanapunda, wenyewe wakawauliza, “Kwa nini mnamfungua mwanapunda huyu?”

34. Nao wakawajibu, “Bwana anamhitaji.”

35. Basi, wakampelekea Yesu yule mwanapunda. Kisha wakatandika mavazi yao juu yake, wakampandisha Yesu juu yake.

36. Yesu akaendelea na safari, na watu wakatandaza mavazi yao barabarani.

37. Alipofika karibu na Yerusalemu, katika mteremko wa mlima wa Mizeituni, umati wote na wanafunzi wake wakaanza kushangilia na kumtukuza Mungu kwa sauti kubwa kwa sababu ya mambo makuu waliyoyaona;

38. wakawa wanasema: “Abarikiwe Mfalme ajaye kwa jina la Bwana. Amani mbinguni, na utukufu juu mbinguni!”

39. Hapo baadhi ya Mafarisayo waliokuwako katika lile kundi la watu wakamwambia Yesu, “Mwalimu, wanyamazishe wanafunzi wako!”

40. Yesu akawajibu, “Nawaambieni, kama hawa wakinyamaza, hakika hayo mawe yatapaza sauti.”

41. Alipokaribia zaidi na kuuona ule mji, Yesu aliulilia

42. akisema: “Laiti ungelijua leo hii mambo yaletayo amani! Lakini sasa yamefichika machoni pako.

43. Maana siku zaja ambapo adui zako watakuzungushia maboma, watakuzingira na kukusonga pande zote.

44. Watakupondaponda wewe pamoja na watoto wako ndani ya kuta zako; hawatakuachia hata jiwe moja juu ya jingine, kwa sababu hukuutambua wakati Mungu alipokujia kukuokoa.”

45. Kisha, Yesu aliingia hekaluni, akaanza kuwafukuza nje wafanyabiashara

Kusoma sura kamili Luka 19