Agano la Kale

Agano Jipya

Luka 10:5-12 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Mkiingia katika nyumba yoyote, kwanza wasalimuni hivi: ‘Amani iwe katika nyumba hii!’

6. Kama akiwako mpenda amani, amani yenu itakaa naye, la sivyo, itawarudieni.

7. Kaeni katika nyumba hiyo mkila na kunywa wanavyowapeni, maana mfanyakazi anastahili mshahara wake. Msiende mara nyumba hii mara nyumba ile.

8. Kama mkifika mji fulani na watu wakiwakaribisha, kuleni wanavyowapeni.

9. Ponyeni wagonjwa walioko huko, waambieni watu: ‘Ufalme wa Mungu umekaribia kwenu.’

10. Lakini mkiingia katika mji wowote, wasipowakaribisheni, tokeni; nanyi mpitapo katika barabara zao semeni:

11. ‘Hata mavumbi ya mji wenu yaliyoshikamana na miguu yetu tunayapangusa dhidi yenu. Lakini, jueni kwamba ufalme wa Mungu umekaribia.’

12. Hakika nawaambieni, siku ile mji huo utapata adhabu kubwa kuliko ile ya watu wa Sodoma.

Kusoma sura kamili Luka 10