Agano la Kale

Agano Jipya

Luka 10:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Baada ya hayo, Bwana aliwachagua wengine sabini na wawili, akawatuma wawiliwawili, wamtangulie katika kila kijiji na mahali ambapo yeye mwenyewe alitaka kwenda.

2. Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini wavunaji ni wachache. Kwa hivyo, mwombeni mwenye shamba atume wavunaji shambani mwake.

3. Sasa nendeni; fahamuni kwamba ninawatuma nyinyi kama kondoo wanaokwenda kati ya mbwamwitu.

4. Msichukue mfuko wa fedha, mkoba, wala viatu; msimsalimu mtu yeyote njiani.

5. Mkiingia katika nyumba yoyote, kwanza wasalimuni hivi: ‘Amani iwe katika nyumba hii!’

6. Kama akiwako mpenda amani, amani yenu itakaa naye, la sivyo, itawarudieni.

Kusoma sura kamili Luka 10