Agano la Kale

Agano Jipya

Luka 1:65-80 Biblia Habari Njema (BHN)

65. Hofu ikawaingia jirani wote, na habari hizo zikaenea kila mahali katika milima ya Yudea.

66. Wote waliosikia mambo hayo, waliyatafakari mioyoni mwao wakisema: “Mtoto huyu atakuwa mtu wa namna gani?” Maana, hakika nguvu ya Bwana ilikuwa pamoja naye.

67. Zakaria, baba yake mtoto, akajazwa Roho Mtakatifu, akatamka unabii huu:

68. “Atukuzwe Bwana Mungu wa Israeli,kwani amewajia na kuwakomboa watu wake.

69. Ametupatia Mwokozi shujaa,mzawa wa Daudi mtumishi wake.

70. Aliahidi hapo kalekwa njia ya manabii wake watakatifu,

71. kwamba atatuokoa mikononi mwa maadui zetuna kutoka mikononi mwa wote wanaotuchukia.

72. Alisema atawahurumia wazee wetu,na kukumbuka agano lake takatifu.

73. Alimwapia Abrahamu babu yetu,kwamba atatujalia sisi

74. tukombolewe mikononi mwa maadui zetu,tupate kumtumikia bila hofu,

75. tuwe wanyofu na waadilifu mbele yake,siku zote za maisha yetu.

76. Nawe mwanangu, utaitwa, nabii wa Mungu Mkuu,utamtangulia Bwana kumtayarishia njia yake;

77. kuwatangazia watu kwamba wataokolewakwa kuondolewa dhambi zao.

78. Mungu wetu ni mpole na mwenye huruma.Atatuchomozea mwanga kutoka juu,

79. na kuwaangazia wote wanaokaa katika giza kuu la kifo,aongoze hatua zetu katika njia ya amani.”

80. Mtoto akakua, akapata nguvu rohoni. Alikaa jangwani mpaka alipojionesha rasmi kwa watu wa Israeli.

Kusoma sura kamili Luka 1