Agano la Kale

Agano Jipya

Luka 1:61-72 Biblia Habari Njema (BHN)

61. Wakamwambia, “Mbona hakuna yeyote katika ukoo wake mwenye jina hilo?”

62. Basi, wakamwashiria baba yake wapate kujua alitaka mtoto wake apewe jina gani.

63. Naye akaomba kibao cha kuandikia, akaandika hivi: “Yohane ndilo jina lake.” Wote wakastaajabu.

64. Papo hapo, midomo na ulimi wake Zakaria vikafunguliwa, akawa anaongea akimsifu Mungu.

65. Hofu ikawaingia jirani wote, na habari hizo zikaenea kila mahali katika milima ya Yudea.

66. Wote waliosikia mambo hayo, waliyatafakari mioyoni mwao wakisema: “Mtoto huyu atakuwa mtu wa namna gani?” Maana, hakika nguvu ya Bwana ilikuwa pamoja naye.

67. Zakaria, baba yake mtoto, akajazwa Roho Mtakatifu, akatamka unabii huu:

68. “Atukuzwe Bwana Mungu wa Israeli,kwani amewajia na kuwakomboa watu wake.

69. Ametupatia Mwokozi shujaa,mzawa wa Daudi mtumishi wake.

70. Aliahidi hapo kalekwa njia ya manabii wake watakatifu,

71. kwamba atatuokoa mikononi mwa maadui zetuna kutoka mikononi mwa wote wanaotuchukia.

72. Alisema atawahurumia wazee wetu,na kukumbuka agano lake takatifu.

Kusoma sura kamili Luka 1