Agano la Kale

Agano Jipya

Luka 1:51-71 Biblia Habari Njema (BHN)

51. Amefanya mambo makuu kwa mkono wake:Amewatawanya wenye kiburi katika mawazo ya mioyo yao;

52. amewashusha wenye nguvu kutoka viti vyao vya enzi,akawakweza wanyenyekevu.

53. Wenye njaa amewashibisha mema,matajiri amewaondoa mikono mitupu.

54. Amemsaidia Israeli mtumishi wake,akikumbuka huruma yake,

55. kama alivyowaahidia wazee wetu,Abrahamu na wazawa wake hata milele.”

56. Maria alikaa na Elisabeti kwa muda upatao miezi mitatu, halafu akarudi nyumbani kwake.

57. Wakati wa kujifungua kwake Elisabeti ulifika, akajifungua mtoto wa kiume.

58. Jirani na watu wa jamaa yake walipopata habari kwamba Bwana amemwonea huruma kubwa, walifurahi pamoja naye.

59. Halafu siku ya nane walifika kumtahiri mtoto, wakataka kumpa jina la baba yake, Zakaria.

60. Lakini mama yake akasema, “Sivyo, bali ataitwa Yohane.”

61. Wakamwambia, “Mbona hakuna yeyote katika ukoo wake mwenye jina hilo?”

62. Basi, wakamwashiria baba yake wapate kujua alitaka mtoto wake apewe jina gani.

63. Naye akaomba kibao cha kuandikia, akaandika hivi: “Yohane ndilo jina lake.” Wote wakastaajabu.

64. Papo hapo, midomo na ulimi wake Zakaria vikafunguliwa, akawa anaongea akimsifu Mungu.

65. Hofu ikawaingia jirani wote, na habari hizo zikaenea kila mahali katika milima ya Yudea.

66. Wote waliosikia mambo hayo, waliyatafakari mioyoni mwao wakisema: “Mtoto huyu atakuwa mtu wa namna gani?” Maana, hakika nguvu ya Bwana ilikuwa pamoja naye.

67. Zakaria, baba yake mtoto, akajazwa Roho Mtakatifu, akatamka unabii huu:

68. “Atukuzwe Bwana Mungu wa Israeli,kwani amewajia na kuwakomboa watu wake.

69. Ametupatia Mwokozi shujaa,mzawa wa Daudi mtumishi wake.

70. Aliahidi hapo kalekwa njia ya manabii wake watakatifu,

71. kwamba atatuokoa mikononi mwa maadui zetuna kutoka mikononi mwa wote wanaotuchukia.

Kusoma sura kamili Luka 1