Agano la Kale

Agano Jipya

Luka 1:42-53 Biblia Habari Njema (BHN)

42. akasema kwa sauti kubwa, “Umebarikiwa kuliko wanawake wote, naye utakayemzaa amebarikiwa.

43. Mimi ni nani hata mama wa Bwana wangu afike kwangu?

44. Nakuambia, mara tu niliposikia sauti yako, mtoto mchanga tumboni mwangu aliruka kwa furaha.

45. Heri yako wewe uliyesadiki kwamba yatatimia yale Bwana aliyokuambia.”

46. Naye Maria akasema,“Moyo wangu wamtukuza Bwana,

47. roho yangu inafurahi kwa sababu ya Mungu Mwokozi wangu.

48. Kwa kuwa amemwangalia kwa huruma mtumishi wake mnyenyekevu.Hivyo tangu sasa watu wote wataniita mwenye heri.

49. Kwa kuwa Mungu Mwenye Nguvu amenifanyia makuu,jina lake ni takatifu.

50. Huruma yake kwa watu wanaomchahudumu kizazi hata kizazi.

51. Amefanya mambo makuu kwa mkono wake:Amewatawanya wenye kiburi katika mawazo ya mioyo yao;

52. amewashusha wenye nguvu kutoka viti vyao vya enzi,akawakweza wanyenyekevu.

53. Wenye njaa amewashibisha mema,matajiri amewaondoa mikono mitupu.

Kusoma sura kamili Luka 1