Agano la Kale

Agano Jipya

2 Wathesalonike 3:13-18 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Lakini nyinyi ndugu, msichoke kutenda mema.

14. Huenda kwamba huko kuna mtu ambaye hatautii huu ujumbe tunaowapelekeeni katika barua hii. Ikiwa hivyo, basi, mfichueni mtu huyo na msiwe na uhusiano wowote naye, kusudi aone aibu.

15. Lakini msimtendee mtu huyo kama adui, bali mwonyeni kama ndugu.

16. Bwana mwenyewe ambaye ndiye chanzo cha amani, awajalieni amani siku zote kwa kila namna. Bwana awe nanyi nyote.

17. Kwa mkono wangu mwenyewe naandika hivi: Salamu kutoka kwa Paulo! Hivi ndivyo ninavyotia sahihi kila barua; ndivyo ninavyoandika.

18. Tunawatakieni nyote neema ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Kusoma sura kamili 2 Wathesalonike 3