Agano la Kale

Agano Jipya

2 Wakorintho 6:13-18 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Sasa nasema nanyi kama watoto wangu: Wekeni mioyo yenu wazi kama nasi tulivyofanya.

14. Msiambatane na watu wasioamini. Je, wema na uovu vyapatana kweli? Mwanga na giza vyawezaje kukaa pamoja?

15. Kristo anawezaje kupatana na Shetani? Mwaamini ana uhusiano gani na asiyeamini?

16. Hekalu la Mungu lina uhusiano gani na sanamu za uongo? Maana sisi ni hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu mwenyewe alivyosema:“Nitafanya makao yangu kwao,na kuishi kati yao.Nitakuwa Mungu wao,nao watakuwa watu wangu.”

17. Kwa hiyo Bwana asema pia:“Ondokeni kati yao,mkajitenge nao;msiguse kitu najisi,nami nitawapokea.

18. Mimi nitakuwa Baba yenu,nanyi mtakuwa wanangu, waume kwa wake,asema Bwana Mwenye Nguvu.”

Kusoma sura kamili 2 Wakorintho 6