Agano la Kale

Agano Jipya

2 Wakorintho 3:11-18 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Maana ikiwa kile kilichokuwa cha muda tu kilikuwa na utukufu wake, bila shaka kile chenye kudumu milele kitakuwa na utukufu mkuu zaidi.

12. Kwa vile hili ndilo tumaini letu, sisi twasema kwa uhodari mkuu.

13. Sisi hatufanyi kama Mose ambaye alilazimika kuufunika uso wake kwa kitambaa ili watu wa Israeli wasiuone ule mwisho wa mngao ule uliokuwa unafifia.

14. Lakini akili zao zilipumbazwa. Mpaka leo hii lisomwapo Agano la Kale, kifuniko hicho bado kipo. Kifuniko hicho kitaondolewa tu mtu anapoungana na Kristo.

15. Naam, mpaka hivi leo kila isomwapo sheria akili zao huwa zimefunikwa.

16. Lakini, wakati mtu amgeukiapo Bwana, kifuniko hicho huondolewa.

17. Hapa “Bwana” ni Roho; na pale alipo Roho wa Bwana ndipo ulipo uhuru.

18. Basi, sisi sote ambao nyuso zetu hazikufunikwa, tunaona kama katika kioo, utukufu wa Bwana; tunabadilishwa tufanane zaidi na huo mfano wake kwa utukufu mwingi zaidi. Hiyo ni kazi yake Roho wa Bwana.

Kusoma sura kamili 2 Wakorintho 3