Agano la Kale

Agano Jipya

2 Wakorintho 2:9-12 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Madhumuni yangu ya kuandika ile barua yalikuwa kutaka kujua kama mko tayari kutii katika kila jambo.

10. Mkimsamehe mtu, nami pia ninamsamehe. Maana ninaposamehe, kama kweli ninacho cha kusamehe, nasamehe mbele ya Kristo kwa ajili yenu,

11. ili tusimpe nafasi Shetani atudanganye; maana twaijua mipango yake ilivyo.

12. Nilipofika Troa kuhubiri Habari Njema ya Kristo, nilikuta mlango u wazi kwa ajili ya kazi ya Bwana.

Kusoma sura kamili 2 Wakorintho 2