Agano la Kale

Agano Jipya

2 Wakorintho 13:8-14 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Maana hatuwezi kuupinga ukweli; uwezo tulio nao ni wa kuuendeleza ukweli.

9. Tunafurahi kwamba sisi tu dhaifu, lakini nyinyi mna nguvu; kwa hiyo tunaomba mpate kuwa wakamilifu.

10. Basi, ninaandika barua hii nikiwa mbali, ili nitakapofika kwenu nisilazimike kuwa mkali kwenu kwa kutumia ule uwezo alionipa Bwana; naam, uwezo wa kujenga na si wa kubomoa.

11. Kwa sasa, ndugu, kwaherini! Muwe na ukamilifu, shikeni mashauri yangu, muwe na nia moja; kaeni kwa amani. Naye Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.

12. Salimianeni kwa ishara ya upendo.

13. Watu wote wa Mungu huku wanawasalimuni.

14. Neema ya Bwana Yesu Kristo na upendo wa Mungu na umoja wa Roho Mtakatifu, viwe nanyi nyote.

Kusoma sura kamili 2 Wakorintho 13