Agano la Kale

Agano Jipya

2 Wakorintho 12:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Nitajivuna basi, ingawa haifai! Lakini sasa nitasema juu ya maono na ufunuo alivyonijalia Bwana.

2. Namjua mtu mmoja Mkristo, ambaye miaka kumi na minne iliyopita alinyakuliwa mpaka katika mbingu ya tatu. (Sijui kama alikuwa huko kwa mwili au kwa roho; Mungu ajua).

3. Narudia: Najua kwamba mtu huyo alinyakuliwa mpaka peponi. (Lakini sijui kama alikuwa huko kwa mwili au kwa roho; Mungu ajua).

4. Huko akasikia mambo ya siri ambayo binadamu hastahili kuyatamka.

Kusoma sura kamili 2 Wakorintho 12