Agano la Kale

Agano Jipya

2 Wakorintho 11:27-33 Biblia Habari Njema (BHN)

27. Nimefanya kazi na kutaabika, nimekesha bila usingizi mara nyingi; nimekuwa na njaa na kiu; mara nyingi nimefunga na kukaa katika baridi bila nguo.

28. Na, licha ya mengine mengi, kila siku nakabiliwa na shughuli za makanisa yote.

29. Kama mtu yeyote ni dhaifu, nami pia ni dhaifu; mtu yeyote akikwazwa, nami pia huwa na wasiwasi.

30. Ikinilazimu kujivuna, basi, nitajivunia udhaifu wangu.

31. Mungu na Baba wa Bwana Yesu – jina lake litukuzwe milele – yeye anajua kwamba sisemi uongo.

32. Nilipokuwa Damasko, mkuu wa mkoa, aliyekuwa chini ya mfalme Areta, alikuwa akiulinda mji wa Damasko ili anikamate.

33. Lakini, ndani ya kapu kubwa, niliteremshwa nje kupitia katika nafasi ukutani, nikachopoka mikononi mwake.

Kusoma sura kamili 2 Wakorintho 11