Agano la Kale

Agano Jipya

1 Wakorintho 9:1-14 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Je, mimi si mtu huru? Je, mimi si mtume? Je, mimi sikumwona Yesu Bwana wetu? Je, nyinyi si matokeo ya kazi yangu kwa ajili ya Bwana?

2. Hata kama kwa watu wengine mimi si mtume, lakini walau kwenu nyinyi mimi ni mtume. Nyinyi ni uthibitisho wa utume wangu kwa sababu ya kuungana kwenu na Bwana.

3. Hoja yangu kwa wale wanaonipinga ndiyo hii:

4. Je, hatuna haki ya kula na kunywa?

5. Je, hatuna ruhusa kumchukua mke Mkristo katika ziara zetu, kama vile wafanyavyo mitume wengine, ndugu zake Bwana, na pia Kefa?

6. Au ni mimi tu na Barnaba ambao tunapaswa kujipatia maslahi yetu kwa kufanya kazi?

7. Je, mwanajeshi gani anayelipia utumishi wake jeshini? Mkulima gani asiyekula matunda ya shamba lake la mizabibu? Mchungaji gani asiyekunywa maziwa ya mifugo yake?

8. Je, nasema mambo haya kibinadamu tu? Je, sheria nayo haisemi hivyo?

9. Imeandikwa katika sheria: “Usimfunge kinywa ng'ombe anapopura nafaka.” Je, ndio kusema Mungu anajishughulisha na ng'ombe?

10. Je, hakuwa anatufikiria sisi aliposema hivyo? Naam, haya yaliandikwa kwa ajili yetu; maana yule anayelima na yule anayevuna, wote wawili wana haki ya kutumaini kupata sehemu ya mavuno.

11. Ikiwa sisi tumepanda mbegu ya kiroho kati yenu, je, ni jambo kubwa tukichuma kwenu faida ya kidunia?

12. Ikiwa wengine wanayo haki ya kutazamia hayo kutoka kwenu, je, sisi hatuna haki zaidi kuliko hao?Lakini, sisi hatukuitumia haki hiyo. Badala yake, tumestahimili kila kitu ili tusiiwekee kizuizi chochote Habari Njema ya Kristo.

13. Je, hamjui kwamba wanaotumikia hekaluni hupata chakula chao hekaluni, na kwamba wanaotoa sadaka madhabahuni hupata sehemu ya hiyo sadaka?

14. Bwana aliagiza vivyo hivyo; wahubiri wa Habari Njema wapate riziki zao kutokana nayo.

Kusoma sura kamili 1 Wakorintho 9