Agano la Kale

Agano Jipya

1 Wakorintho 3:15-23 Biblia Habari Njema (BHN)

15. lakini kama alichojenga kitaunguzwa, basi, atapoteza tuzo lake; lakini yeye mwenyewe ataokolewa kana kwamba ameponyoka kutoka motoni.

16. Je, hamjui kwamba nyinyi ni hekalu la Mungu, na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?

17. Basi, mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu; maana hekalu la Mungu ni takatifu, na hekalu hilo ni nyinyi wenyewe.

18. Msijidanganye! Mtu yeyote miongoni mwenu akijidhania mwenye hekima mtindo wa kidunia, heri awe mjinga kusudi apate kuwa na hekima ya kweli.

19. Maana, hekima ya kidunia ni upumbavu mbele ya Mungu. Kwani Maandiko Matakatifu yasema: “Mungu huwanasa wenye hekima katika ujanja wao.”

20. Na tena: “Bwana ajua kwamba mawazo ya wenye hekima hayafai.”

21. Basi, mtu asijivunie watu. Maana kila kitu ni chenu.

22. Paulo, Apolo na Kefa, ulimwengu, maisha na kifo; mambo ya sasa na ya baadaye, yote ni yenu.

23. Lakini nyinyi ni wa Kristo, naye Kristo ni wa Mungu.

Kusoma sura kamili 1 Wakorintho 3