Agano la Kale

Agano Jipya

1 Wakorintho 2:5-9 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Nilifanya hivyo kusudi imani yenu ipate kutegemea nguvu ya Mungu, na si hekima ya binadamu.

6. Hata hivyo, sisi tunatumia lugha ya hekima kwa wale waliokomaa kiroho; lakini hekima hiyo si ya hapa duniani, wala si ya watawala wa dunia hii ambao wako katika mkumbo wa kupotea.

7. Hekima tunayotumia ni hekima ya siri ya Mungu, hekima iliyofichika, ambayo Mungu aliiazimia tangu mwanzo kwa ajili ya utukufu wetu.

8. Ni hekima ambayo watawala wa dunia hii hawakuielewa; maana wangaliielewa, hawangalimsulubisha Bwana wa utukufu.

9. Lakini, ni kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:“Mambo ambayo jicho halijapata kuyaona,wala sikio kuyasikia,mambo ambayo binadamu hajapata kuyafikiria moyoni,hayo ndiyo Mungu aliyowatayarishia wale wampendao.”

Kusoma sura kamili 1 Wakorintho 2