Agano la Kale

Agano Jipya

1 Wakorintho 16:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Sasa, yahusu ule mchango kwa ajili ya watu wa Mungu: Fanyeni kama nilivyoyaagiza makanisa ya Galatia.

2. Kila Jumapili kila mmoja wenu atenge kiasi cha fedha kadiri ya mapato yake, ili kusiwe na haja ya kufanya mchango wakati nitakapokuja.

3. Wakati nitakapokuja kwenu, nitawatuma wale mtakaowachagua miongoni mwenu wapeleke barua na zawadi zenu Yerusalemu.

4. Kama itafaa nami niende, basi, watakwenda pamoja nami.

5. Nitakuja kwenu baada ya kupitia Makedonia – maana nataraji kupitia Makedonia.

6. Labda nitakaa kwenu kwa muda fulani, au huenda nitakaa pamoja nanyi wakati wote wa baridi, ili mpate kunisaidia niendelee na safari yangu kokote nitakakokwenda.

7. Sipendi kupita kwenu harakaharaka na kuendelea na safari. Natumaini kukaa kwenu kwa kitambo fulani, Bwana akiniruhusu.

8. Lakini nitabaki hapa Efeso mpaka siku ya Pentekoste.

Kusoma sura kamili 1 Wakorintho 16