Agano la Kale

Agano Jipya

1 Wakorintho 14:9-17 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Hali kadhalika na nyinyi, kama ulimi wenu hausemi kitu chenye kueleweka, nani ataweza kufahamu mnayosema? Maneno yenu yatapotea hewani.

10. Zipo lugha mbalimbali ulimwenguni, na hakuna hata mojawapo isiyo na maana.

11. Lakini ikiwa mimi sifahamu maana ya lugha asemayo mtu fulani, mimi ni mgeni kwake mtu huyo naye pia ni mgeni kwangu.

12. Hali kadhalika na nyinyi, maadamu mna hamu ya kupata vipaji vya Roho, jitahidini hasa kujipatia vile vinavyosaidia kulijenga kanisa.

13. Kwa hiyo, mwenye kunena lugha ngeni na aombe apate uwezo wa kuzifafanua.

14. Maana, nikisali kwa lugha ngeni roho yangu ndiyo inayosali, lakini akili yangu hubaki bure.

15. Nifanye nini, basi? Nitasali kwa roho yangu, nitasali pia kwa akili yangu; nitaimba kwa roho yangu, nitaimba pia kwa akili yangu.

16. Ukimsifu Mungu kwa roho yako tu, atawezaje mtu wa kawaida aliye katika mkutano kuitikia sala yako ya shukrani kwa kusema: “Amina”, kama haelewi unachosema?

17. Sala yako ya shukrani yaweza kweli kuwa bora, lakini huyo mwingine haitamfaidia.

Kusoma sura kamili 1 Wakorintho 14