Agano la Kale

Agano Jipya

1 Wakorintho 14:32-40 Biblia Habari Njema (BHN)

32. Kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu ni lazima kitawaliwe na huyo mwenye hicho kipaji.

33. Maana Mungu si Mungu wa fujo, ila wa amani.

34. Kama ilivyo desturi katika makanisa yote ya watu wa Mungu, wanawake wakae kimya katika mikutano ya waumini. Hawana ruhusa kusema; ila wawe watii kama isemavyo sheria.

35. Ikiwa wanayo maswali ya kuuliza, wawaulize waume zao nyumbani, maana ni aibu kwa mwanamke kusema katika mikutano ya waumini.

36. Je, mnadhani neno la Mungu limetoka kwenu nyinyi au kwamba limewajieni nyinyi peke yenu?

37. Kama mtu yeyote anadhani kwamba yeye ni mjumbe wa Mungu au kwamba anacho kipaji cha Roho, na ajue kwamba haya ninayowaandikia nyinyi ni amri ya Bwana.

38. Lakini mtu asiyetambua hayo, basi, mtu asimjali mtu huyo.

39. Hivyo basi, ndugu zangu, mnapaswa kuwa na hamu ya kutangaza ujumbe wa Mungu; lakini msimkataze mtu kusema kwa lugha ngeni.

40. Lakini yote yafanyike kwa heshima na kwa utaratibu.

Kusoma sura kamili 1 Wakorintho 14